MCHANGO WA TAFSIRI KATIKA UKUAJI WATAMTHILIA YA KISWAHILI.
UTANGULIZI:
Dhana ya tafsiri
na tamthiliya kuswahili:
Catford (1965:20) anasema tafsiri ni kuchukua mawazo
yaliyo katika maandishi kutoka lugha moja (lugha chanzi) na kuweka badala yake
mawazo yaliyolingana katika lugha nyingine (lugha lengwa).
Mwansoko, (2006) anafasili neno tafsiri ni zoezi la
kuhawilisha ujumbe kutoka matini chanzi kwenda matini lengwa.
Kwa mujibu wa Wafula, (1999).Anaeleza kuwa kuna aina
nne za tamthiliya zilizo tafsiriwa kama ifuatavyo, kwanza kuna tamthiliya
zilizo tafsiriwa kutoka lugha nyingine hadi kiingereza na kisha kutafsiriwa kwa
Kiswahili,mfano wa tamthiiya hizo ni pamoja na “mchuuzi muungwana”yake
Moliere, nyingine ni “Mfalme Edipode”
yake Mbunda Msokile na ile ya “Mkaguzi
Mkuu wa Serikali” yake Nikolai Gogol.
Pia kuna zile tamthilia zilizo andikwa kwa kiingereza
na wageni na kutafsiriwa kwa Kiswahili mfano wa tamthilia ilizo tafsiriwa
katika mfumo huu ni pamoja na tamthiliya zote za Shake speare.Vilevile kuna
tamthiliya zilizoandikwa asilia kwa kiingereza na Waafrika kisha zikatafsiriwa
kwa Kiswahili. “Maswaibu ya Ndugu Jero”
na “Mzalendo Kimathi” ni mifano ya tamthiliya. Kuna tamthilia zilizoandikwa
katika lugha nyingine za kiafrika na kutafsiriwa katika Kiswahili mfano wa
tamthilia ni “Nitaolewa Nikipenda”.
Hivyo kwa ujumla, tunaweza kusema kuwa tafsiri ni
kitendo cha kufikisha ujumbe wa matini chanzi katika matini lengwa kwa
kuzingatia muundo wa lugha lengwa na maana ya lugha lengwa.
Tamthiliya ya Kiswahili ni ile tamthilia inayojadili
mambo mbalimbali yahusuyo utamaduni wa waswahili na iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
Mfano; “Kaptula la Maksi” yake
Euphrase Kezilahabi na “Safari ya Chinga”yake
Shani Omary.
Tafsiri ni nyenzo muhimu sana katika kukuza na
kusambaza fasihi. Tafsiri ndilo daraja linalounganisha jamii za watu wanaotumia
lugha zinazotofautiana.
MCHANGO WA TAFSIRI
KATIKA UKUAJI WATAMTHILIA YA KISWAHILI.
Kwa mujibu wa mwansoko na wenzake (2006) wanasema
shughuli za wazalendo zimejadiliwa na mashirika ya utafsiri na uchapishaji ya
nchi za nje ambayo yamefanya kazi kubwa ya kupanua hazina ya vitabu vya
Kiswahili.
Baadhi ya mashirika hayo ni; shirika la uchapaji lugha
za kigeni, Beijing China, miongoni mwa tafsiri za Kiswahili za mashirika haya
ni pamoja na shajara ya mwenda wazimu na hadithi teule za lu kun.
Kutokana na maendeleo ya tafsiri fasihi ya Kiswahili
imesambaa na kuwafikia watu wa mataifa mbalimbali.
Kwa mujibu wa Ruhumbika, (1978) anasema kuwa waandishi
wengi wamejifunza mbinu za uandishi wa tamthiliya kutoka mataifa mengine. Mfano
wa mbinu hizo ni kama vile mtindo, ujenzi
wa wahusika na uundaji na ubunifu wa mandhari na mbinu nyinginezo za
kisanaa.
Mbinu hii tafsiri imefanya fasihi ya Kiswahili kukua
na kuweza kuendelea kufanyiwa ulinganisho na fasihi nyingine za ulimwengu,
mfano: tamthiliya ya “Amezidi” ya
Said A. Mohamed. Mfano wa kazi zilizotafsiriwa; aliyeonja pepo, nitaolewa
nikipenda yake ngugi wa thiong’o,” Adui
wa Umma “na “Orodha”.
Vilevile
tafsiri imesaidia kuendeleza fasihi ya Kiswahili na utamaduni wake katika jamii
tofautitofauti kwa mfano, kuna kazi za fasihi ya Kiswahili zikiwemo tamthiliya
za Kiswahili zilizotafsiriwa ambazo ni pamoja na; “Tufani” ya Samweli S. Mushi, “Shetani
Msalabani”, “Mtawa Mweusi”na
“Nitaolewa nikipenda” zake Ngugi wa Thiong’o.
Pia taaluma ya tafsiri imesaidia kuongezeka kwa
machapisho mengi ya kazi za Tamthiliya, hii imefanyika hasa mara baada ya kazi
nyingi za tamthiliya kutafsiriwa kutoka lugha nyingine nakutafsiriwa katika
lugha ya Kiswahili,mfano wa kazi zilizo tafsiriwa na kuongeza idadi kubwa ya
machapisho ni pamoja na “Adui wa
Umma”,”Mkaguzi wa serikali” na “Nitaolewa nikipenda”.kazi zote hizi
zimesaidia katika kuendeleza ukuaji na kusambaa kwa tamthiliya.
Pia tafsiri inakuza lugha ya fasihi husika, kupitia
tafsiri msamiati mpya unaingia katika lugha husika tukijua kuwa lugha ndio
mhimili wa fasihi, kwa hiyo msamiati ukiimarika fasihi pia huimarika.
‘Lugha nyingi za kiafrika Kiswahili kikiwa miongoni
mwao hazikuwa zimeendelea sana kimaandishi hasa maandishi ya kufasili, kwa hiyo
tafsiri za tamthilia zikilenga kukuza maandishi ya lugha za Kiswahili. Na
vilevile tamthilia ilitafsiri kwa lengo la kuongeza machapisho ya fasihi ya
kiswahili’’ (Ruhumbika 1978).
Method (2015) anasema kuwa kazi za tafsiri zina mchango
mkubwa sana katika ukuaji wa fasihi ya Kiswahili,tamthilia ikiwemo. Fasihi ya
kiingereza inaonekana kunufaika sana kutokana na tafsiri ya fasihi za Kiyunani,
Kiroma, Kirusi na Kifaransa (Wafula 1999:13) Ryanga (1985) katika makala yake
iliyoitwa vitabu vya kutafsiriwa na
fasihi ya Kiswahili. Anasema kuwa tafsiri ina dhima kimaudhui na kifani katika
fasihi ya Kiswahili na fasihi nyinginezo. Kimaudhui anabainisha kuwa aina mpya
ya maudhui huweza kuibuka katika fasihi lengwa. Kifani anazitaja faida za kazi
za tafsiri katika fasihi ya Kiswahili kuwa ni pamoja na kuibuka kwa mitindo
mipya ya uandishi na kuingia kwa tanzu mpya katika fasihi ya Kiswahili.
Faida nyingine
tunazoweza kuziongezea hapa ni pamoja na kutia shime na kuendeleza uandshi wa
kifasihi, kupanua hadhira ya kazi ya fasihi,kuongeza msamiati wa lugha na
kadhalika. Kabla ya kuzama sana na kuweza kubainisha na kuchambua kazi za
tafsiri katika tamthilia ya Kiswahili ni vema kwanza tufafanue kwa kina dhima
hizi za tafsiri.
Tukianza na dhima ya kimaudhui, tumesema kwamba
tafsiri imeweza kuibua aina mpya ya maudhui. Hii ina maana kuwa kazi
inapotafsiriwa kutoka jamii lugha ambayo imepiga hatua kubwa kimaendeleo
kunakuwa na maudhui mapya ambayo yanaweza kuingizwa katika fasihi lengwa hivyo
kuweza kuamsha ari ya kimapinduzi. Kwa mfano inapotokea jamii yenye
ukandamizaji wa wanawake ila haina mwamko wa kupinga ukandamizaji huo wa
wanawake, jamii lengwa huwez kupata mwamko na kujifunza kwamba kukomeshwa kwa
ukandamizwaji wa wanawake ni jambo linalowezekana.
Kwa upande wa dhima za kifani, tunaona kwamba kazi za
tafsiri katika fasihi ya Kiswahili huweza kuibua mitind mipya ya uandishi.
Jamii huweza kutofautiana na huweza pia kuwa na mitindo mbalimbali ya utunzi na
uandishi wa kifasihi. Hivyo, kazi ya fasihi inapotafsiriwa kutoka jamii moja
kwenda nyingine, jamii lengwa hunufaika na mitindo ya uandishi iliyopo katika
jamii chanzi. Katika tafsiri uzingalifu wa mitindo ni jambo la muhimu sana.(Mwansoko
na wenzake 2006).
Pia tafsiri huweza kusababisha kuingia kwa tanzu mpya
katika fasihi lengwa. Kama inavyobainishwa na wataalamu mbalimbali, tanzu za
fasihi hutofautiana kutoka jamii moja kwenda nyingine (Samwel 2012, Samwel na
wenzake 2013). Hivyo kazi fulani ya fasihi inapotafsiriwa kutoka katika jamii
moja kwenda nyingine ambayo haina utanzu husika, jamii lengwa hunufaika kwa
kuweza kupata aina mpya ya utanzu. Fasihi ya Kiswahili kwa mfano
imenufaishwa sana na utanzu wa tanzia ambao umeingizwa katika fasihi hiyo
kutokana na kazi za tafsiri za kifasihi kama vile Oedipus the king (Sophocles) ambayo imetafsiriwa Kiswahili, Maflme Edipode ((S. Mushi).
Katika dhima ya kutia shime na kuendeleza uandishi wa
kifasihi tunaona kuwa tafsiri imeweza kuwatia moyo waandishi na kuweza kuandika
zaidi. Mwandishi wa kifasihi anapoona kuwa kazi yake imetafsiriwa katika lugha
nyingine na kuoana hadhira pana, hummotisha kutunga zaidi. Aidha kutokea
mwandishi akaandika kazi yake ya fasihi na kukosa soko katika jamii
aliyoikusudia kutokana na sababu kama vile kukosekana kwa mwamko wa usomaji,
umaskini, ukosefu wa elimu na kadhalika. Katika hali kama hiyo, mwandishi
husika atanufaika na soko la nje kutokana na tafsiri na hivyo kutokata tama kuandika
zaidi.
Dhima nyingine tuliyobainisha ni kupanua hadhira ya
kazi ya fasihi. Kazi ya fasihi napotafsiriwa hupanua hadhira ya kazi ya
kifasihi. Kazi hiyo hupata hadhira pana zaidi na hivyo maudhui yake kuwafikia
watu wengi zaidi kuliko kama isingetafsiriwa katika lugha nyinginezo. Maudhui
ya kazi ya fasihi huwalenga watu, hivyo, kama kazi husika itakuwa na hadhira
finyu, mchango wa kazi hiyo katika ukombozi wa jamii huwa mdogo pia.
Vilevile tafsiri huongeza msamiati wa lugha. Husemwa
kwamba jamii lugha hutofautiana katika mambo mbalimbali ikiwa pia ni utamaduni
wa kiwango cha maendeleo kilichofikiwa. Kazi ya fasihi ya jamii iliyopiga hatua
kubwa kimaendeleo inapotafsiriwa, huweza kusaidia jamii lugha yenye maendeleo
duni kuongeza msamiati. Msamiati wa lugha hutegemeana na kiwango cha maendeleo
kilichofikiwa. Lugha ya Kiswahili imenufaika sana na kazi hizi za tafsiri. Pia
hudaiwa kuwa lugha kama haitumiki haikui, hivyo kutafsiri kutaifanya lugha
itumike hivyo kukua.
HITIMISHO.
Hivyo basi kazi ya tafsiri ni nyenzo kubwa katika
kuenezana kukuza faasihi ya Kiswahili zikiwemo tamthilia ya Kiswahili kwani
kutokana na kazi ya kutafsiriwa kutoka lugha mbalimbali huifanya lugha hiyo
ikue kwa kuongeza misamiati na idadi ya watumiaji pamoja machapisho ya kifasihi
ambayo hupelekea kukua na kuendelea kwa fasihiya Kiswahili.
MAREJELEO.
Catford J.C (1965).
A linguistic translation theory of:
An easy in applied linguistics. London: Oxford press.
Method, S.(2015).Umahiri Katika Fasihi ya Kiswahi,
Mwongozo Kwa Mwanafunzi na Mwalimu wa
Fasihi Simulizi na Andishi. Meveli Publishers (MVP).
Mwansoko H.J.M na
wenzake (2006). Kitangulizi cha Tafsiri:
Nadharia na mbinu. Dar-es-salaam: TUKI.
Ruhumbika, G. (1978). Tafsiri za kigeni katika ukuzaji wa fasihi ya Kiswahili. Makala.
Wafula, R.M
(1999).Uhakiki wa tamtiliya,
Historian a maendleo yake . Nairobi Kenya: Jomo Kenyatta Foundation.
No comments