Fasili ya neno kileksika, kimuundo na kisarufi
DHANA ZA MSINGI
(a)
Mofimu
Kwa
mujibu wa Matinde (2012:101) mofimu ni maana inayowakilishwa na mofu. Pia
mofimu ni dhana ambayo ni sehemu ya umilisi kwa watumiaji wa lugha husika.
Mofimu
ni vipashio vidogo vya msingi vinavyotumika katika kuunda maneno ya lugha.
Mofimu ni vipashio vinavyoonyesha uhusiano uliopo kati ya sauti msingi za lugha
yaani fonimu na maana maalumu katika sarufi ya lugha (Besha, 1994:52).
Aidha
Massamba na wenzake (2013:13) wanaeleza kuwa mofimu ni kipashio kidogo kabisa
katika umbo la neno kilicho amilifu (yaani kilicho na kazi ya kisarufi au
kileksika) na ambacho hakiwezi kuvunjwa au kugawanywa katika vipande vingine
vidogo bila kupoteza uamilifu wake.
Kwa
ujumla mofimu ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana kisarufi au kileksika.
Aina za Mofimu
Matinde
(2012) ameainisha na kuelezea aina kuu mbili za mofimu yaani mofimu huru na
mofimu tegemezi.
Mofimu
huru. Ni silabi moja au zaidi yenye maana kamili ya neno na inaweza kujisimamia
yenyewe bila msaada wa viambishi au silabi nyingine. Aghalabu mofimu huru huwa
nomino, vivumishi au vielezi visivyochukua viambishi vya ngeli mfano daktari,
ndoa, nyumba.
Mofimu
tegemezi. Ni mofimu ambazo huhitaji viambishi ili kukamilisha maana
iliyokusudiwa. Mofimu hizi hujumuisha mzizi wa neno au shina la kitenzi,
kivumishi, nomino au vielezi ambavyo vinahitaji viambishi viwakilishi vya ngeli
ili kutoa maana iliyokusudiwa.
Kwa
ujumla mofimu inaweza kujidhihirisha kwa namna kuu tatu tofautitofauti ambazo
ni;
(i)
mzizi. Mfano; ruk- ruka
Kop-
kopa
Pig-
piga
Lim- lima
Chez- cheza
(ii)
kiambishi. Mfano; a-na-temb-e-a
a-na-lim-a
kop-esh-a
a-na-chez-a
(iii)
Neno yaani neno sharti liwe linajitosheleza kimaana mfano Baba, Dirisha, Mama, Kaka, Babu, Asha,
Juma na maneno mengineyo mengi ya namna hiyo.
(b) Alomofu
Matinde
(2012:100) Alomofu ni maumbo mawili au zaidi yanayowakilisha mofimu moja na hutokea
katika mazingira maalum ya utokeaji.
Besha
(1994:55) anaeleza kuwa Alomofu za mofimu ambazo zinatokea katika mazingira
maalumu ya kifonolojia ya utokeaji wake unaweza kutabirika.
Hivyo
basi, Alomofu ni maumbo mawili au zaidi yanayowakilisha mofimu ileile moja na
ambayo huweza kutokea katika mazingira maalum.
Kanuni za alomofu katika kauli ya
kutendeka.
Matinde
(2012:192) anasema kuwa alomofu {-ik-} hutokea katika shina likiwa na irabu
mojawapo kati ya a, i au u na mzizi huo huishia na konsonanti ambayo huonyesha
ubora wa jambo fulani au uwezekano wa kitu kufanyika.
Mfano;
{imb-} + //-ik-// + {-a} = imbika
{umb-} + //-ik-// + {-a} = umbika
{fany-} + //-ik-// + {-a} = fanyika
{pit-} + //-ik-// + {-a} = pitika
{tup-} + //-ik-// + {-a} = tupika
Habwe
na Karanja (2007:110) anasema alomofu /-ek-/ hutokea iwapo mzizi wa kitenzi
ndani yake una irabu e au o na mzizi huo huishia na konsananti na huonyesha
ubora wa kitu/jambo kufanyika au uwezekano wa jambo fulani kufanyika.
Mfano; {jeng-} + //-ek-// + {-a} =jengeka
{pony-} + //-ek-// + {-a} =
ponyeka
{chom-} + //-ek-// + {-a} =
chomeka
{tosh-} + //-ek-// + {-a} =
tosheka
{som-} + //-ek-// + {-a} =
someka
{tek-} + //-ek-// + {-a} =tekeka
(c) Mofu
Matinde
(2012) akiwanukuu TUKI (1990) wanaeleza kuwa mofu ni kipashio cha isimu maumbo kiwakilishacho
mofimu.
Matinde
(2012) Mofu ni umbo kamili ambalo huwakilisha mofimu. Umbo hilo hudhihirika
kifonolojia na kiothografia (uwezo wa kutamkwa na kuandikwa).
Katika
lugha ya kitaalamu umbo linalowakilisha mofimu hujulikana kama mofu (Massamba
na Wenzake, 2013:14).
Kwa
ujumla mofu ni umbo au maumbo yanayowakilisha mofimu na ambayo yanaweza
kudhihirika kwa kutamkwa au kimaandishi.
Aina za Mofu
Matinde
(2012) ameainisha mofu kwa kuzingatia vigezo viwili ambavyo ni:
(i) kigezo cha isimu maana
(ii) kigezo cha isimu maumbo
Katika
kigezo cha isimu maana tunapata aina kuu tatu za mofu ambazo ni;
(i) Mofu huru
(ii) Mofu funge
(iii) Mofu tata
(i)
Mofu huru
Ni
mofu ambazo zinaweza kukaa peke yake kama maneno kamili yenye maana
inayoeleweka bila kusaidiwa na mofu nyingine. Mofu huru zinaweza kuwa nomino, kivumishi, kiwakilishi, kielezi, kitenzi au kiunganishi.
(ii)
Mofu funge au tegemezi
Ni
mofu ambayo haiwezi kukaa peke yake kama neno lenye maana kamili. Mofu hizi
huhitaji kuambatanishwa na mofu nyingine ili kupata maana sawa au neno kamili.
Mfano: M-toto – w-atoto
Ki-su – vi-su
M-ti
– mi-ti
Ji-tu – ki-ji-tu
Wakati
mwingine mofu funge inaweza ikatokea katika mizizi ya vitenzi:
Mfano: {-l-} katika neno kula
{-f-} katika neno kufa
{lim-} katika neno lima
{-j-} katika neno kuja
{-nyw-} katika neno kunywa
(iii)
Mofu tata
Ni
mofu ambayo huwa na maana zaidi ya moja yaani kuanzia mbili na kuendelea.
Mofimu tata hutokea katika vitenzi vilivyopo katika kauli ya kutendea.
Mfano:
Alimpigia = a-li-m-pig-i-a.
Alimchezea = a-li-m-chez-e-a.
Alimchomekea = a-li-m-chom-ek-e-a.
Hivyo
mofu {-i-} na {-e-} ni mofu ambazo zinaonyesha kauli ya kutendea na ndizo
zinaleta utata katika vitenzi hivyo.
Kigezo cha isimu maumbo
Matinde
(2012) anaeleza kuwa katika kigezo hiki cha isimu maumbo kuna aina kuu mbili za mofu. Aina hizo
za mofu ni;
(i) Mofu changamani
(ii) Mofu kappa
(i)
Mofu changamani
Ni
mofu inayoundwa kutokana na mwambatano wa mizizi miwili ambayo inaweza ikawa ni
mizizi sahihi miwili kama vile;
{Askari} + {Kanzu} = Askarikanzu
{Gari} + {Moshi} = Garimoshi
{Fundi} + {Chuma} = Fundichuma
Pia
inaweza ikawa mofu funge + mofu huru
Mfano:
{Mw-} + {-ana} + {nchi} = Mwananchi
{Mw-} + {-ana} + {hewa} =
Mwanahewa
(ii)
Mofu kapa
Ni
mofu za pekee ambazo hazina umbo. Mofu kapa hazitamkwi wala kuandikwa. Mofu
kapa hazionekani katika neno lakini athari zinazotokana na mofu kapa hueleweka.
Mfano; Umoja wingi
U-kucha – ⱷkucha
U-kuta –
ⱷkuta
U-funguo - ⱷfunguo
Nomino
zilizo na kiambishi cha wingi tu cha umoja hakipo
Mfano;
umoja wingi
ⱷkasha Ma – kasha
ⱷdebe
Ma – debe
ⱷjembe
Ma – jembe
(b) Fasili ya neno kileksika, kimuundo na
kisarufi
(i) Fasili ya neno Kileksika
Neno
ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana. Kwa maana hiyo neno ni lazima liwe
na maana inayoeleweka kwa jamii inayotumia lugha hiyo. (Mdee, 1977).
Mfano: Mama-
Mzazi wa kike
Ndama-
Mtoto wa ng`ombe
Dhana
hii ina mashiko kwa sababu maneno mengi katika lugha yana maana ya kueleweka
kwa watumiaji wa lugha.
Udhaifu
wa fasili hii
Si
kila neno linalotumika linaweza kuwa na maana ya wazi au ya kileksika. Mfano
baadhi ya maneno hasa viunganishi na
vihusishi kama vile ya, kwa, na, wakati ambapo yanakua hayana
maana ya kileksika lakini yana uamilifu kisarufi.
(ii) Fasili ya neno kimuundo
Neno
ni kipengele kidogo kabisa cha sentensi ambacho kinaweza kuhamishwa kutoka
nafasi moja hadi nyingine bila kuathiri sarufi ya lugha katika tungo au sentensi
hiyo (cruse, 1986) akinukuliwa na (Mdee, 1997). Kwa ujumla hapa kinachotazamwa zaidi ni
kategoria za maneno na mpangilio wake katika tungo.
Mfano:
Ali alimuua Ahmed
N T
N
Ahmed alimuua Ali
N T
N
Hapa
N ni nomino na T ni kitenzi japo nomino zimebadilishana nafasi lakini sarufi
hiyo haijaathirika. Utaratibu huu husaidia katika kujifunza sarufi ya lugha
hasa miundo ya tungo kama kirai, kishazi na sentensi na pia kujua sehemu za
tungo kama kiima na kiarifu.
Udhaifu
wa fasili hii
·
Sio maneno yote yanaweza
kuhamishwahamishwa bila kuvuruga sarufi ya lugha
Mfano;
Ali
alisimama kando ya mto
Amesimama
kando ya mto Ali
Kando
ya mto Ali amesimama
*Mto
Ali amesimama kando ya
*Mto
ya kando amesimama
Hivyo
sentensi mbili za mwisho hazikidhi haja ya usahihi wa kisarufi.
·
Vilevile unapohamisha maneno basi maana ya
neno pia hubadilika.
Mfano; Zubeda anampenda Zawadi
Zawadi
anampenda Zubeda
Nomino
zimebadilishana nafasi hazijaathiri sarufi ya lugha lakini kimaana imebadilika
kwa sababu katika sentensi ya kwanza Zubeda ndiye anatenda tendo na katika
sentensi ya pili Zawadi ndiye anatenda tendo.
(iii)
Fasili ya neno kisarufi
Kwa mujibu wa Katamba (1993:19) ili neno
litambulike lazima liwe katika muktadha wa matumizi. Katamba anasema neno moja
linaweza kuwa na dhima mbalimbali na dhima hiyo itagundulika tu litakapokuwa
ndani ya muktadha wa matumizi kwenye sentensi. Anatoa mfano wa neno la
kiingereza “cut” kwamba likiwa kipwekepweke mtu hawezi kutambua linarejelea
nini pamoja kwamba neno hilo katika lugha ya kiingereza ni kitenzi yaani ‘kata’
lakini kuna wakati linaweza kutumika kurejelea nomino. Mfano I need my cut na I
have cut my fingure. Ukichunguza vizuri mifano hii ‘cut’ katika sentensi ya
kwanza hurejelea nomino na katika sentensi ya pili hurejelea kitenzi. Sentensi
ya kwanza ilikuwa na maana ‘nahitaji stahiki yangu’ na ya pili ina maana ya
‘nimekata kidole’.
Kigezo
hiki huenda mbali kwa kufafanua kuwa pia maneno kama ‘na’, ‘tu’, ‘si’ katika
Kiswahili na maneno kama ‘and’, ‘an’, ‘the’ ‘on’ katika kiingereza nayo
hayawezi kutambulika yanarejelea nini, lazima yawe katika muktadha wa matumizi
ndio tunaweza kusema ni aina gani za maneno na kutambua maana zake.
Udhaifu
wa fasili hii
Si
lazima maneno yote yawe katika muktadha wa matumizi ndipo tuweze kubaini maana
zake kwani kuna baadhi ya maneno huweza kutambulika kuwa yana maana gani hata yasipokuwa katika muktadha wa matumizi
katika sentensi. Kwa mfano nomino za mahali kama vile Dodoma, Mwanza na
Morogoro na majina ya watu kama vile Amina, Omari, Magreth na Ali.
HITIMISHO
Hivyo
basi katika kufasili dhana ya neno ni vyema kuzingatia vigezo vyote vya
kisarufi kama vile fonolojia, maana, sarufi ili kupunguza changamoto
zinazojitokeza katika kufasili dhana hii kama ilivyobainishwa hapo juu.
MAREJELEO:
Besha, R.M. (2007). Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dar es Salaam: Macmillan Aidan
Ltd.
Habwe, J. & Karanja, P. (2007). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi:
Phoenix Publishers.
Katamba, F. (1993). Morphology. London: Macmillan Press Ltd.
Massamba, D.P.B na Wenzake. (2013). Fonolojia
ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI.
Matinde, R.S. (2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia: Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo
Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publishers (T) Ltd.
Mdee, D. (2007). Nadharia za Leksikografia. Dar es Salaam: TUKI.
TUKI. (1990). Kamusi ya Isimu na Lugha. Dar es Salaam:
TUKI
Nawapa Sana kongore kwa juhudi mnazozionyesha katika lugha yetu hii ya kiswahili kwa lengo la kukikuza Kama ishara pia kuwaenzi wasisi wetu ambao walikitumia Sana na hata kutuachia Kama urithi wa Leo na hata kesho.
ReplyDelete