UNYAMBULISHAJI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
UTANGULIZI.
Maana ya unyambulishaji
Massamba
(2009:105), unyambulishaji ni utaratibu wa kupachika viambishi kwenye mizizi
ili kuunda maneno mapya.
Unyambulishaji
ni mbinu ya uundaji wa maneno,hivi kwamba viambishi mbalimbali huambikwa kwenye
mzizi husika na kuunda neno jipya.(Matinde,2012:119).
Unyambulishaji
ni utaratibu katika lugha wa kupachika au kuongeza viambishi kwenye mzizi wa
neno ili kuunda maneno mapya. Kwa mfano, kuunda nomino kutokana na vitenzi kwa
kutumia viambishi. Maneno mapya yanayoundwa hapa huwa ya kategoria nyingine
(Masebo,2012:127).
Hivyo
basi tunaweza kusema kwamba unyambulishaji ni aina ya uambishaji unaosababisha
neno kutoka katika kategoria moja hadi nyingine.
Unyambulishaji wa nomino
Habwe
na Kalanje (2004),wanadai kuwa unyambulishaji wa nomino ni hali ya kuunda
nomino kutoka kuwa kategoria nyingine za maneno huitwa unominishaji. Nomino za
Kiswahili zinaweza kuundwa kutokana na vitenzi, vivumishi na hata kutokana na
nomino moja hadi nyingine.
Hivyo
basi, unyambulishaji wa nomino ni hali ya kuweka viambishi vinyambulishi kwenye
mzizi wa neno ambao hupelekea neno hilo kuhama kutoka kategoria moja kwenda
kategoria nyingine ambayo ni nomino.
Nomino.
Ni
neno linalotaja kitu, kiumbe, hali, dhana au tendo kama kiti,ndege na furaha. (Massamba,
2009:68).
Unyambulishaji
wa nomino hufanyika kama ifuatavyo;
Kinominishi
{o} kinaweza kunominisha vitenzi vya Kiswahili katika mazingira yafuatayo;
Kwa
mfano vitenzi vya kibantu vinavyoishia na kiambishi tamati {-a}
{Mzizi}
+ {-o}
Mfano,
Kitenzi
mzizi nomino
Tenda tend +o tendo
Andika andik + o andiko
Jenga jeng + o jengo
Pamba pamb + o pambo
Hata
hivyo, kuna baadhi ya vitenzi vya kibantu ambavyo huishia na kiambishi tamati
{-a} ambavyo vikiambikwa viambishi tamati {-o} haviwezi kubadilika na kuwa
nomino. Kwa mfano kitenzi ;Lowa,tembea.
Pia
kiambishi cha unyambulishi {-o} huweza kunyambulisha nomino kwa kuambatana na
kinyambulishi {-i} au {-li}.
kwa
mfano; {mzizi} + {-i/-li-} + {-o}
Kitenzi mzizi nomino
Kaanga kaang + i + o kaangio
Chuja chuj + i + o chujio
Kaa ka + li + o kalio
Mazingira
mengine kiambishi kinyambulishi {o} huweza kunominisha kitenzi pale ambapo
huambatana na mofimu {e}.
{mzizi}
+ {-e-} + {-o}
Kwa
mfano; Kitenzi mzizi nomino
Fyeka
fyek + e + o fyekeo
Chekecha chekech + e + o chekecheo
Pia
unyambulishaji wa nomino huweza kutokea kwa kuambika kiambishi {M-/Mw-}
mwanzoni kabla ya shina la kitenzi na
kiambishi cha unyambulishi {-ji} baada ya mzizi wa neno. Kiambishi tamati {-ji}
cha unominishaji ambacho huonesha mtu anayetenda kitendo kama kazi yake ya kila
siku.
{M/Mw-}+{shina-T}+{-ji}
Mfano
kitenzishinanomino
Baka m + baka + ji mbakaji
Chezam + cheza + ji mchezaji
Imba mw+imba+ji mwimbaji
Omba mw +omba + jimwombaji
Nomino
zenye mofolojia yenye kiambishi awali {ku}, ambacho hutumiwa kuunda nomino.
Kiambishi hiki {ku} huwekwa mbele ya shina la kitenzi na hubadili kitenzi kuwa
nomino.
{Ku-}
+ {shina-T}
Mfano,
Kitenzi shina nomino
imba ku
+ imba kuimba
Cheza ku
+ cheza kucheza
Lia ku + lia kulia
Piga ku + piga kupiga
Nomino
zenye mofolojia yenye kiambishi awali {u} cha unominishaji , mzizi wa kitenzi
na kiambishi tamati {vu/fu} cha unominishaji. Huonyesha mtu au watu walio
katika hali fulani.
{u}
+ {MZIZI} + {vu/fu}
Mfano:-
Kitenzi Mzizi Nomino
Tulia u + tuli + vu Utulivu
Vumilia u + vumili + vu Uvumilivu
legea
u + lege + vu Ulegevu
Nomino
zenye mofolojia yenye kiambishi awali {ki} cha unominishaji katika umoja au
{vi} katika umoja , mzizi wa kitenzi na kiambishi tamati {o} kiambishi hiki huweza kuleta dhana
ya kitu/ kifaa kinachotumika kutenda kitendo.
{Ki/ Vi} + {MZIZI} + {o}
Mfano:-
Kitenzi Mzizi Nomino
Funika
ki + funik + o kifuniko/vifuniko
Pima
ki + pim + o kipimo/vipimo
Tua
ki + tu + o kituo/vipimo
Kiambishi
kinyambulishi {-a}
Ikiwa
kitenzi huishia kwa irabu i au u irabu hizo hubadilika na mahali pake huchukuliwa
na kiambishi tamati {a} hivyo husababisha kitenzi kubadili kategoria yake na
kuwa nomino.
Yaani,
{mzizi} + {a}
Mfano,
Kitenzi mzizi nomino
Hoji hoj + a hoja
Faidi faid + a faida
Heshimu heshim + a heshima
Unyambulishaji katika vitenzi
Rubanza
Y.I (1996), unyambulishaji wa vitenzi ni upachikaji wa mofimu fuatishi katika
vitenzi.
Kitenzi
ni neno ambalo huarifu tendo linalofanyika. TUKI (2012).
Mgullu
(2012),anadai kuwa katika lugha ya Kiswahili vitenzi vinaweza kuundwa kutokana
na vivumishi.
Kwa
mfano;
Refu
refusha
Fupi
fupisha
Bora
boresha
Safi safisha
Pia
mara chache sana nomino zikinyambuliwa huunda vitenzi, Masebo (2012:134).
Kwa
mfano;
Nomino Kitenzi
Taifa taifisha
Sulubu sulubisha
Ratiba ratibu
Hata
hivyo kuna idadi ndogo ya vielezi vikinyambuliwa vinaweza kutumikakatika kuunda
vitenzi. Kwa mfano;
Kielezi Kitenzi
Haraka harakisha, harakishwa,
HITIMISHO.
Unyambulishaji
wa maneno katika lugha ni muhimu sana katika ukuaji wa lugha kwani hupelekea
kuongezeka kwa misamiati katika lugha.
MAREJELEO.
Habwe
na Karanja, (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Foenix Publishers.
Massebo
(2012). Nadharia ya Lugha Kiswahili
1,kidato cha 5&6.Dar Es salaam: Nyambari
Matinde,
S. (2012), Dafina ya Lugha Isimu na
Nadharia, kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo
Mgullu,
(2012), Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia
ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers.
Nyangwine
Publishers.
TUKI
(2012). Kamusi ya Kiswahili Sanifu.
Dar Es salaam: Oxford University Press.
Vikuu. Mwanza: Serengeti
Educational Publishers.
Ipo vizuri
ReplyDeleteiko poah
ReplyDeleteImekaa poa
ReplyDeleteIna fana sana
ReplyDeleteUjumbe mzuri
ReplyDelete