KUFANANA NA KUTOFAUTIANA KWA MOFOLOJIA NA FONOLOJIA
FASILI ZA DHANA ZA FONOLOJIA
MOFOLOJIA
FONOLOJIA:
Fonolojia ni tawi la Isimu ambalo
hushughulikia uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha. (Massamba na wenzake.
(2001:183).
Fonolojia hushughulikia vipashio ambavyo
hutumika katika lugha inayohusika. (Massamba na wenzake (2001:183).
Kwa fasili hizo tunaweza kusema kuwa
Fonolojia ni tawi la Isimu ambalo hujishughulisha na uchambuzi wa mfumo wa
sauti katika lugha inayohusika.
MOFOLOJIA:
Mofolojia ni tawi la Isimu ambalo
hujishughulisha na uchambuzi wa kanuni na mifumo inayohusu upangaji wa mofimu
mbalimbali ili kuunda maneno katika lugha. Massamba na wenzake (2001:192).
Mofolojia ni kiwango muhimu cha lugha
ambacho hujushughulisha na mpangilio wa vipande sauti vyenye maana. (Bakari, M.
(1988:18).
Kwa fasili hizo tunaweza kusema kuwa
Mofolojia ni tawi la Isimu linalojishughulisha na kanuni na mifumo ya upangaji
wa mofimu katika kuunda maneno.
KUSIGANA
KWA TAALUMA YA MOFOLOJIA NA FONOLOJIA:
Umbo la msingi la mofolojia hujulikana
kama mofu ilihali umbo la msingi la fonolojia ni fonimu. Mofu ni maumbo yanayowakilisha Mofimu na
Fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia kinachojihusisha na lugha
mahsusi. Mifano:
FONIMU ZA KISWAHILI NA KIPARE
|
MOFU ZA KISWAHILI
|
MOFU ZA KIPARE
|
-m, n, t, k, g, l, v
-i, e, a, o, u
Hizi ni baadhi ya fonimu katika lugha za
kibantu kikiwemo Kiswahili na Kipare).
|
m – toto
wa – toto
m – ni mofu funge ya umoja
wa – ni mofu funge ya wingi
toto – ni mofu huru.
|
mwa-na
va-na
mwa – mofu funge ya umoja
va – mofu funge ya wingi
|
Matawi ya Mofolojia hutofautiana na matawi
ya fonolojia. Hii ni kutokana na kwamba
matawi ya Mofolojia ni Mofolojia ya minyumbuliko ya maneno na Mofolojia ya
uundaji wa maneno ilihali katika fonolojia kuna Fonolojia vipande na fonolojia
arudhi.
Matawi ya Mofolojia hushughulika zaidi na
mbinu za uundaji wa maneno ilihali matawi ya fonolojia kuhusika na sauti za
lugha mahsusi, namna ya utamkaji na vipamba sauti kwa ujumla.
Fonolojia hushughulikia muainisho wa
vipashio vya lugha inayohusika, jinsi vipashio hivyo vinavyofuatana na
kuathiriana ilihali mofolojia huhusika na maumbo ya maneno yenye maana kisarufi
na jinsi yanavyoweza kuathiriana. Mifano
ifuatayo hudhihirisha muathiriano wa kimofolojia na kifonolojia. Rubanza I. Y.
(1996:3-4).
KIFONOLOJIA
|
KIMOFOLOJIA
|
||
SAUTI
|
SILABI
|
MOFIMU
|
NENO
|
/p/ /t/ /a/ /g/ /i/ /o/
|
pa + ta + ga + gi + pi + go
|
pat – a
pig – o
pat – o
pit – a
|
pata
pigo
pato
pita
|
Katika mifano hiyo ni dhahiri kuwa sauti
huungana ili kuunda silabi hususani muunganiko wa konsonanti na irabu katika
kuunda silabi ilihali mofimu huungana ili kuunda neno.
KUSHABIHIANA
KWA TAALUMA YA FONOLOJIA NA MOFOLOJIA:
Kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya
fonolojia na uundaji wa maneno katika lugha yoyote iwayo. Wanaendelea kusema kuwa, kwa upande wa
mofolojia, maneno huundwa na mofimu na mofimu huundwa na sauti. Aidha uundaji wa mofimu hufuata taratibu
maalum za mfuatano wa sauti za lugha ihusikayo. Massamba na wenzake (2013:14).
Tuchunguze mifano ifuatayo katika lugha ya
Kiswahili na lugha ya Kipare:
SAUTI
|
MOFIMU
|
MANENO
|
-
/p/ + /a/ + /t/ + /a/
-
/i/ + /m/ + /b/ + /a/
-
/k/ + /a/ + /t/ + /a/
-
/b/ +/i/+/g/+ /h/ + /a/
-
i + m + a
-
e + i + m + b + a
|
pat – a
imb – a
kat – a
bigh – a
im – a
e – imb – a
|
pata (kiswahili)
imba (kiswahili)
kata (kiswahili)
bigha (kipare – piga)
ima (kipare – lima)
eimba (kipare – anaimba).
|
Taaluma ya fonolojia na mofolojia zina
uhusiano na zinategemeana. Rubanza Y.I. (1996:4). Anasema, uhusiano wa karibu
wa folonojia na mofolojia unadhirika kutokana na mifano ifuatayo:-
Kushoto: Kulia:
a)
Mu
– ana = mwana
b)
Mu
– anafunzi = mwanafunzi
c)
Mu
– alimu = mwalimu
Kipashio [mu-] katika jozi ya kushoto
kinachodhihirisha umoja hujitokeza kama [mw-] katika jozi ya kulia, ambapo
kanuni hiyo inazingatia taaluma ya kifonolojia na mofolojia. Kanuni hiyo ni mu → mw - /- I ikimaanisha
[mu-] inajitokeza kama [mw-] inapofuatwa na irabu ambapo katika mifumo hiyo ni
irabu [-a-]
i → y / -
+ a. Sheria hii inatuambia kuwa irabu juu inayotamkiwa mbele hubadilika
na kuwa kiyeyusho kinachoendana nayo iwapo mbele yake kutakuwa na irabu chini
inayotokea baada ya mpaka wa mofimu. Massamba,
(2012:19).
Mifano:
-
Kiswahili:
vi+ama = vyama
Vi+ake = vyake
Vi+ao = vyao
-
Kipare: vi + avo = vyavo (vya kwao).
Vi + enyu = vyenyu (vya kwenu).
Uundaji wa mofimu za lugha ambao ni sehemu
za mofolojia hufuata taratibu maalum za fonolojia ya lugha inayohusika. Hii ndiyo maana tunasema kwamba kuna uhusiano
wa moja kwa moja baina ya mofolojia na fonolojia. Tuchunguze mfuatano wa sauti zifuatazo ambazo
utaratibu wa fonolojia ya Kiswahili haukubali pamoja na lugha zingine za
kibantu na kupelekea kuundwa kwa maandishi yasiyo na maana. Massamba na wenzake
(2013:15)
SAUTI ZENYE MPANGILIO USIOKUBALIKA
|
UMBO LISILOKUBALIKA
|
MPANGILIO UNAOKUBALIKA
|
|
Sauti
|
Neno
|
||
/g/
/k/ /a/ /i/ /p/ /i/
/b/ /b/ /b/ / u/ /u/
/a/ /k/ /k/ /g/ /o/
|
gkaipi
bbbu
akkgo
|
/p/ /i/ /g/ /i/ /k/ /a/
/b/ /u/ /b/
/u/
/k/
/a/ /g/ /o/
|
pigika
bubu
kago
|
Vipashio vya kifonolojia ndivyo viundwavyo
vipashio vya kimofolojia. Hii ina maanda
kuwa muunganiko wa sauti za lugha zikiwemo konsonanti, viyeyusho na Irabu hunda
silabi na silabi huunga na kuunda maneno ambapo kimsingi uundaji wa sauti na
silabi hufanyika kifonolojia ili kuunda mofimu kisha maneno ambayo ni
mofolojia. (Rubanza Y. I. (1996:4).
MIFANO YA SAUTI
|
SILABI
|
MOFIMU
|
NENO (MAANA)
|
Kiswahili = /a//n//a//c//h//z//a/
Kiswahili= /w//a//m//e//f//u//a/
Kipare = /e//c//h//e//z//a/
Kipare = /v//a//f//u//a/
|
a+na+che+za
wa+me+fu+a
e+chez+a
va+fu+a
|
a-na-chez-a
wa-me-fu-a
e-chez-a
va-fu-a
|
Anacheza
Wamefua
Echeza (anacheza)
Vafua (wamefua)
|
Vilevile kwa upande wa Fonolojia silabi ni
kipashio cha kiisimu ambacho hutamkwa kwa mara moja kama fungu la sauti linalojitegemea. Katika mtazamo huihuo tunaweza kusema mofimu
ni kipashio kidogo kabisa katika umbo la neno ambacho hakiwezi kuvunjwa na
kugawanywa katika vipande vingine bila kupoteza uamilifu wake. Massamba na wenzake, (2013:13). Tuchunguze
mifano ifuatayo:
SILABI
|
IDADI
|
MOFIMU
|
IDADI
|
pi + ga + ni + sha
pa + ta
di + ri + sha
|
(silabi nne)
(silabi mbili)
(silabi tatu)
|
pi – ga – ni – sha
pa – ta
dirisha
|
(mofimu nne)
(mofimu mbili)
(mofimu moja)
|
Taaluma ya fonolojia inahusisha silabi
huru na silabi funge jambo ambalo mofolojia nayo ina mofimu huru na mofimu
funge. Silabi huru ni silabi zinazoishia na irabu ilihali silabi funge ni
silabi zinazoishia na consonant. Hali
kadhalika mofimu huru ni mofimu zinazojitosheleza kimaana ilihali mofimu funge
ni zile mofimu ambazo hutegemea mofimu zingine katika neno ili ziweze
kujitosheleza kimaana.
Mifano:-
SILABI
HURU SILABI FUNGE:
Kiswahili: -
ba + ba = baba Kiingereza
= father (baba)
-
a + mu + a = amua = fax (faksi)
Kipare -
va + va = vava (baba) = sector (sekta)
-
a + mu + a = amua
Mofimu
huru Mofimu
funge
-
Fluri
a
+ na + lim + a
-
Lea
A
= huwakilisha nafasi ya tatu umoja.
-
Rozina
na
= huwakilisha wakati.
lim = mzizi wa
neno.
a = mofimu tamati.
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kwamba
taaluma ya fonolojia na Mofolojia ni matawi ya kiisimu ambayo hutegemeana kwa
kiwango kikubwa katika kujenga lugha hususani muunganiko wa sauti katika
kujenga silabi, muunganiko wa silabi kuunda mofimu na muunganiko wa mofimu
katika kuunda maneno.
MAREJELEO:
Dr.
Bakari, M. (1988). Analysis of Modern
Swahili Texts and Language Skills. Nairobi: University of Nairobi.
Kyao,
R. (1988). Kiswahili Sekondari. TUMI.
Massamba
na wenzake, (2001). Sarufi Miundo ya
Kiswahili Sanifu. Dar es salaam. TUKI.
Rubanza
Y.I. (1996). Mofolojia ya Kiswahili.
Dar es salaam. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
jjk
ReplyDeleteKazi nzuri mashallah
ReplyDeletekazi bora ya utafiti
ReplyDelete