swali;Eleza Athari ya viambishi vinyambulishi
Maana
ya Viambishi:
Kutokana na Riro S. Matinde katika
kitabu chake cha Dafina ya Lugha na
Nadharia, (2012). Anasema; “Kiambishi
hutokana na neno ambika ambapo kuambika ni kuweka kitu mahali kwa kukiegemeza
kwa kingine”. Hivyo basi anaendelea
kusema kuwa; “Viambishi ni vineno vilivyoshikishwa katika mzizi wa kitenzi,
kabla na hata baada ya mzizi wa kitenzi hicho”.
Hivyo basi tunaweza kusema kuwa
viambishi ni maneno yanayowekwa mwanzoni au mwishoni mwa kitenzi na kuleta
maana fulani. Pia tunaweza kusema kuwa
kiambishi ni silahi inayofungamanishwa na mzizi wa neno, kwa hiyo kiambishi ni
Mofimu Tegemezi.
Riro S. Matinde anaendelea kusema
kuwa kuna aina mbili za viambishi ambavyo ni:-
(1) Viambishi
Awali – hivi ni viambishi ambavyo hutokea mwanzoni mwa Kitenzi (kabla ya mzizi)
na huwa vya aina mbalimbali.
(2) Viambishi
Tamati – Hivi ni viambishi ambavyo hutokea mwishoni mwa Kitenzi (baada ya
mzizi).
Viambishi vya
Mnyambuliko:
Vitenzi hunyumbuliwa au kurefushwa kwa
kuongezwa viambishi ambavyo hudokeza kauli mbalimbali kati ya Kitenzi na
Kiishio. Viambishi hivi vya mnyambuliko
ni viambishi ambavyo hutokea baada ya mzizi wa kitenzi. Huwa upande wa kulia wa mzizi. Matinde anaeleza kuwa Viambishi hivi huwa na
uamilifu ufuatao:
(a) Kiishio
hicho ni kiambishi ambacho hutokea mwishoni mwa Kitenzi, aghalabu {a} hutokea
katika vitenzi vinavyotokana na lugha za kibantu ilihali {e}au {i} au {u}
hutokea katika vitenzi vyenye asili ya lugha za kigeni, mathalani ingia,
ongoza, vua, starehe, ahidi, sahau na vinginevyo vingi.
(b) Virejeshi
– virejeshi hutumika kulingana na ngeli za nomino, viambishi hivi hutuelekeza
kwa mtenda au mtendwa katika baadhi ya vitenzi.
Kwa
mfano:
(i)
Vibaka wasumbuao mjini wmeongezeka mara
dufu.
(ii)
Akufukuzaye hakwambii toka.
(iii)
Kimsumbuacho ni urembo wake.
(iv)
Amwambiaye uongo ni bibi yake.
Kwa
maana hiyo tunaweza kusema kuwa viambishi vya mnyambuliko wa vitenzi hubadilika
Kisintaksia kulingana na mnyambuliko wa vitenzi. Kwani kama inavyojulikana kuwa
Sintaksia ni tawi la Isimu linalojishughulisha na maumbo mbalimbali ya maneno.
Kutokana
na maelezo hayo hapo juu tunaweza kusema kwamba athari za viambishi
vinyambulishi katika kitenzi zinaweza kuonekana katika kauli mbalimbali kama
ifuatavyo:
(i)
Kuali ya kutendea.
(ii)
Kauli ya kutendewa .
(iii)
Kauli ya kutendana .
(iv)
Kauli ya kutendesha.
(i) Kauli
ya kutendea – Kauli hii huonyesha hali ya kumfanyia mtu/kitu jambo fulani, na
hapa atahari ya kiambishi huonekana pale ambapo Kitenzi hunyambuliwa au
hurefushwa. Kwa mfano:
·
Soma – som-e-a.
·
Imba – imb-i-a.
·
Cheza – chez-e-a.
·
Osha – osh-e-a
(ii) Kauli
ya kutendewa – Kauli hii huonyesha mtu / kitu kufanyiwa jambo fulani na
mtu/kitu mwininge na athari ya kiambishi huonekana kama ifuatavyo:-
·
Weka – wek-ew-a.
·
Lima – Lim-iw-a.
·
Lipa – Lip-iw-a.
·
Beba – beb-ew-a.
(iii) Kauli
ya kutendana – Hii ni ile hali ya kumfanya mtu kitendo naye anakufanya hivyo
hivyo:
Mfano:
·
Piga – pig-an-a.
·
Pika – piki-a-na.
·
Omba – omb-a-n-a.
·
Fanya – fany-a-n-a.
(iv) Kauli
ya kutendesha – Hii ni ile hali ya kumfanya mtu atende jambo Fulani. Mfano wa athari za vitenzi vinyambulishi
katika kauli hii ya kutendesha ni kama ifuatavyo:
·
Andika – andik-ish-a.
·
Lima – lim-ish-a.
·
Cheza – chez-esh-a.
·
Soma – som-esh-a.
Hivyo
basi kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa viambishi vinyambulishi vina athari
katika vitenzi kwani huonyesha kauli mbalimbali. Pia ambapo vitenzi huyambuliwa au kurefusha.
Mnaeleweka Sana.
ReplyDelete